Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakazi wa eneo la Jogoo, mjini Kisii wameitaka serikali ya Kaunti ya Kisii kujenga matuta katika sehemu hiyo ya barabara linalotoka Kisii kuelekea Nyamira kuzuia visa vya ajali kuendelea.

Haya yanajiri baada ya wanafunzi wawili kugongwa na kujeruhiwa vibaya na waendeshaji bodaboda katika visa tofauti siku ya Jumatatu na Jumanne. 

Wakazi hao wakiongozwa na mmoja wa chama cha wafanyibiashara katika eneo hilo Johnstone Omwoyo, siku ya Jumanne jioni baada ya mwendeshaji bodaboda kumgonga mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Jogoo ilioko kando ya barabara hilo, wliwashtumu baadhi ya vijana wa bodaboda ambao wanaendesha bodaboda yao kwa kasi bila kujali watoto wadogo ambao huvuka barabara hilo wakielekea shuleni.

Kwa upande wake Verah Kerubo ambaye ana kibanda cha kuuza mboga na matunda katika eneo hilo, alimwomba Waziri wa barabara kusaidia kuweka matuta na pia kuweka sheria mahususi za kuwathibiti hasa wahudumu wa bodaboda na madereva wa magari aina ya Probox ambayo alisema yamekuwa yakisababisha ajali katika barabara hilo mara kwa mara.

"Serikali ya kaunti ituwekee matuta ili madereva wa magari pamoja na bodaboda waweze kupunguza mwendo wao wa kasi ambao zimesababisha kugongwa kwa watu na hata wenginekufariki na kuachwa vilema," alisema Kerubo.

Hata hivyo mmoja wa kiongozi wa steji ya bodaboda sehemu hiyo Sebastian Oraro aliwatetea waendeshaji bodaboda akisema kuwa hua wanafuata sheria za barabara huku akiwalaumu wanaotumia barabara hilo kwa kutokuwa makini wanapovuka barabara.