Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa Matunwa katika Wadi ya Gesima wamewaonya vijana wanao tabia ya kuwaibia ndizi kutoka shambani mwao kukoma.

Wakiongea siku ya Jumapili na Mwaadishi huyu katika eneo la Matunwa, Kaunti ya Nyamira, wakazi hao ambao ni wakulima wa vyakula mbali mbali ikewemo ndizi walisema kuna baadhi ya vijana ambao wanawahangaisha kwa kuiba ndizi hizo huku wakiwaonya kuwa siku zao zinahesabiwa.

Aidha, wamemwomba chifu wa Lokesheni ya Mochenwa Magara Makori kuitisha Baraza ili kutoa tangazo hilo kwa watu wote haswa kwa vijana hao kabla ya wakazi wa eneo hilo kuchukua mkondo mwingine.

Wakazi hao walidai kuwa vijana hao huiba ndizi hizo kabla ya kukomaa na kuwaacha wakulima hao bila mazao

"Tumekuwa tukisumbuliwa na wezi hao hasa wakati huu tunapotegemea ndizi kwa kuunza na kununua chakula nyingine kufuatia mahindi kukataa kumea," ahihoji Sheila Kerubo, mkulima.

Salome Mokeira mkulima mwingine naye alisema kuwa umbali wa shamba lake kutoka nyumbani mwake, wezi hao wamekuwa wakimsumbua kila wakati.

Kwa sasa wakazi hao wametangaza hali hatari kwa wezi hao na kusema wamechoshwa nao huku mzee wa Kijiji hilo Nyakwana Orogo akiahidi kuhakikisha kuwa wezi hao watanaswa.