Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa Kaunti ya Kisii wameshauriwa kufika katika vituo vya afya katika mji wa Kisii kujua hali yao ya afya kila kuchao.

Akiongea na wakazi wa mtaa wa Mwembe siku ya Jumapili, mhudumu wa afya ya Jamii katika Kaunti ya Kisii Kepha King’oina aliwaambia wakazi hao kuwa kuna umuhimu wa kila mkazi kuenda hospitali kila kuchao ili kujua hali yake ya afya.

King’oina alisema kuwa kujua hali ndio njia pekee itakayoweza kusaidia watu kujua njinsi ya kujingika kutoka na maradhi mbalimbali katika jamii akiongeza kuwa mtu anapoenda hospitalini sio kupimwa tu, bali anapewa mawaidhaa jinsi ya kujingika kutokakna na magonjwa mbalimbali.

Aidha, aliwasahuri vijana kutopuuza masharti wanaopewa kutoka kwa madaktari na kuwaomba vijana hao kufika katika vituo vya afya ili kujua hali ya afya bila kuogopa.

Kwa mujibu wa mhudumu huyo, watu wengi hupuuza kuenda katika vituo vya afya kwa kuhofia kuwa aidha akipatikana na ugonjwa wowote itakuwa mwisho wa maisha yake.

Pia aliwahimiza kuwa bora kinga kuliko dawa kwani katika hospitali kuna mawaidha yatakayo wasaidia vijana kujiendeleza kimaisha hata iwapo watapatikana na ugonjwa wowote ule.

“Kuna umuhimu mkubwa wa kuenda katika hospitali ili kujua hali yetu ya kiafya kwani ni busara kujijua na kujikinga kutokana na maradhi mabaya na vile vile kuyakubali matokeo na kuishi na ugonjwa wowote ule iwapo mmoja atapatikana nayo,” aliongezea King’oina.