Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakazi kutoka Kaunti ya Kisii wameshauriwa kupanda nyasi aina ya mabingobingo ambazo ni imara ili kuzuia mmomonyoko wa udongo wakati wa mvua ya El Nino.

Akizungumza siku za Jumanne katika ofisi yake wakati wa kikao cha kujadili mwafaka na utaratibu wa kupigana na mvua ya El Nino ambayo inatarajiwa kuanzia mwezi wa Octoba, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Kilimo katika kaunti ya Kisii, Nathan Soire, aliwataka wakulima kuchukua nafasi ya mapema kabla ya mvua hiyo kuanza kunyesha na kupanda nyasi hiyo kando kando ya mashamba yao.

Alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuhifadhi rotuba ya mashamba kwani nyasi hizo zitazuilia udongo kubebwa na maji hali ambayo itapoteza rotuba.

Soire pia aliwashauri wakulima kujiepusha na kuchimbua au kulima mashamba yao kwa kiwango kilichozidi, na kushauri wakulima kuchimba mitaro ambayo itasaidia kuweka maji ya mvua katika mkondo ambao utayaelekeza maji hayo kwenye vidimbwi au kwenye mito badala za kuyaruhusu kuingia katika mashamba, kwasababu maji mengi hudhoofisha mimea.

“Wakazi pia wanapaswa kupanda aina nyingine ya mimea ambayo husaidia kuhifadhi udongo kama vile mboga aina ya mchicha, ambayo ni thabiti.