Share news tips with us here at Hivisasa

Baada ya wanaoishi na ulemavu katika Kaunti ya Nyamira Kuandamana kulalamikia kutopata ajira katika kaunti hiyo, sasa wametakiwa kutuma maombi ya ajira ili kuajiriwa na serikali ya kaunti hiyo.

Wakiongozwa na katibu wao, Jared Wilberforce, walilalamikia kubaguliwa kwa kutopewa kazi zinazotolewa katika kaunti hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumapili mjini Nyamira, katibu huyo alisema aliandaa kikao na karani wa kaunti hiyo, Erick Aori, kuzungumzia swala la wanaoishi na ulemavi kutoajiriwa.

Alisema kuwa karani huyo aliwaomba wale wanaohitaji kazi katika kaunti hiyo kutuma maombi ya ajira chini ya wiki moja ijayo ili kuajiriwa.

Tangazo hilo liliopokelewa kwa furaha huku wanaoishi na ulemavu wakisema kuwa wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu lakini juhudu zao zimefua dafu sasa.

“Nilizungumza na karani wa kaunti yetu ya Nyamira na akasema wale wanaohitaji ajira watume maombi na watapata ajira kulingana na katiba,” alisema Wilberforce.

Aliongezea, “Niko na furaha kubwa kwani kubaguliwa kwetu kumefika mwisho na tutapata ajira kama watu wanaoishi na ulemavu wa kaunti hii ya Nyamira.”