Share news tips with us here at Hivisasa

Tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) imekosolewa na wapiga kura kutoka eneo la Bonchari katika uteuzi wa mwakilishi.

Hii ni baada ya mwakilishi wa wadi kutoka eneo la Bochari kwa jina Muslima Dida kuteuliwa kuwa mwakilishi mteule katika bunge la kaunti ya kisii kupitia chama cha UDF. Wapiga kura hao wamesema uteuzi huo ulikuwa kinyume cha sheria.

David Ogega na Jared Osano Atancha walielekea katika Mahakama ya Kisii siku ya Jumanne kupinga kuteuliwa kwa mwakilishi huyo wakisema jina la mwakilishi huyo halikuwa katika orodha ya majina ya watu yaliyowasilishwa kwa tume hiyo.

Wamesema kuwa mwakilishi huyo amekuwa akipokea mshahara wa bure kutoka kwa serikali ya kaunti ya Kisii. Sasa wawili hao wanataka mwakilishi huyo na mwingine kuteuliwa.

Walifikisha mashtaka hayo kwa mahakama ya Kisii kupitia wakili wao Joshua Obebo. Tarehe rasmi ya kusikizwa kwa kesi hiyo bado haijatangazwa na mahakama.