Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mkuu wa idara ya afya katika Kaunti ya Nyamira Douglas Bosire amesema zahanati zote zilioko kwa kaunti hiyo ambazo hazitimizi mahitaji ya sekta ya afya na hazina vyeti vya kuruhusu kufanya kazi hiyo zitafugwa karibuni.

Wito huo umetolewa baada ya kubainika kuwa zahanati nyingi hazina vyeti na wale wanauza dawa katika zahanati hizo za kibinafsi hawajahitimu kufanya kazi hiyo.

Bosire alisema msako mkali utaanzishwa na serikali ya Kaunti ya Nyamira na zahanati hizo kufungwa.

Akiongea na waandishi wa habari siku ya Jumanne katika mji wa Nyamira, Bosire alisema serikali ya Nyamira haitaruhusu zahanati ambazo hazifuati sheria kuendelea na kazi.

“Serikali yetu ina mpango wa kuweka sheria kamili maana imebainika zahanati nyingi ziko na watu ambao hawajahitimu na hawana vyeti. Hivi karibuni tutaweweka sheria ambazo lazma zifuatwe na tutaanza msako ili kufunga zahanati hizo,” alisema Bosire.

Aliongeza, “Mara nyingi tunapoanzisha msako wa aina hiyo huwa wanafunga zahanati hizo na hatutaendelea kuona maisha ya watu yakiwa hatarini. Lazima tuzingatie sheria za sekta ya afya ili watu wasiathiriwe.”

Bosire amewomba wenye zahanati hizo kufuata yale yanahitajika ili kupata idhini ya kuendelea kufanya kazi hiyo.