Afisa mmoja wa GSU amefikishwa katika mahakama ya Molo kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 3.
Kulingana na kiongozi wa mashtaka Evalyne Ndegwa, Boniface Muenga, ambaye ni afisa wa GSU wa kambi ya Jolly Farm wilayani Molo, alitekeleza uovu huo baada ya kuachwa pekee yake kwenye kambi hiyo majira ya mchana.
Kiongozi huyo wa mashtaka alisema mtoto huyo alipata majeraha mabaya baada ya kitendo hicho kulingana na ripoti ya dakatari.
Mshukiwa alikabiliwa na mashtaka mawili, moja likiwa kosa la ubakaji pamoja na kumchapa na kuumiza mfanyakazi wa nyumba ambaye aliachiwa jukumu la kutunza mtoto huyo wakati wa tukio.
Mahakama ilielezwa kwamba mshukiwa alimdunga kisu mfanyikazi huyo baada yake kudai kwamba ataripoti kisa hicho.
Mshukiwa amekana mashataka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili ama pesa taslimu Sh 100,000.
Hakimu mkazi Rita Amwahi amesema kesi hiyo itatajwa Januari 29, 2016 na kusilikizwa Februari 6.