Share news tips with us here at Hivisasa

Akina mama wanaofanya biashara ya miraa mjini Garissa wamelalamikia kupotea kwa miraa yao inapofika katika maeneo ya wakimbizi ya Hagadera na viunga vyake.

Walipokuwa wakiongea na wanahabari wakiwa kwenye vituo vya mabasi ya kusafirisha miraa mjini Garissa, wamama hao walisema kuwa wamechoka kuona miraa yao ikipotea hivyo kuwalazimu kujitokeza na kulalamikia kwa wakuu wa mabasi ya kusafirisha miraa. 

“Hakuna faida tunayopata katika biashara hii ya miraa. Kila siku tunalipa shilingi 200 au hata 500 kwa kila gunia na miraa inapofika katika maeneo tunalokusudia, tunaambiwa kuwa miraa yetu imepotea na hivyo basi kutopata faida yoyote” alisema  Buthul Sareyo, mmoja wa wamama hao.

Wamama hao wanaeleza kuwa biashara hiyo ya miraa ndilo wanalotumia nalo kukidhi mahitaji ya watoto wao kwa kuwasomesha na vile vile kuwalea.

“Hatuna njia nyingine ya kulisha watoto wetu kwa mahitaji yao mbalimbali kama vile kuwalipia karo na kwa matibabu yao,” mama mwengine walisema.