Mbunge wa Nakuru Magharibi Samwel Arama amelitaka bunge la kaunti ya Nakuru kupitisha sheria zitakazo walinda makahaba kutokana na mauaji.
Akizungumzia swala la mauaji ya makahaba mjini Nakuru, Arama alisema kuwa ukahaba si mbaya na kutaka makahaba watengewe sehemu maalum ya kuendeleza biashara yao bila kusumbiliwa.
Akizungumza na wanahabari mjini Nakuru Jumapili, Arama alisema ni hatia kuwaua watu wamaofanya kazi yao kutafuta riziki.
Alitoa mfano wa taifa la India ambapo biashara hiyo imehalalishwa na kutaka hilo lifanyike Nakuru.
“Mimi nimetembelea India na huko hii biashara ya ukahaba imehalalishwa na na watu wameruhusiwa kuifanya katika maeneo fulani na hata hapa Nakuru tunataka sheria ya kuwaruhusu hawa wasichana kufanya kazi yao,” Arama alisema.
“Ukahaba si mbaya kwani unahusisha mwanamke na mwanamme na bunge la kaunti ni lazima lifanye kitu kuwakinga hawa wasichana,” aliongeza.
Naye mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri alitaka majumba yote yanayotumiwa na makahaba kuweka rekodi za watu wote wanaoingia humo ili kuweza kuwatambua wahalifu wanaowaua makahaba kwa urahisi.
“Kama haya majumba ya starehe yangeweka orodha ya watu wanaoingia na makahaba humo basi ingekuwa rahisi kuweza kuwakamata wahalifu,” Ngunjiri alisema.