Askari jamii (community police) mjini Mombasa wameonywa dhidi ya kuwanyanyasa wananchi kwa kisingizio cha kuwahudumia raia.
Onyo hii imetolewa na Naibu Kamshina wa Kaunti ya Mombasa Salim Mahmoud.
Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumamosi, Mahmoud alisema kuwa hatau za kisheria zitachukuliwa dhidi ya askari jamii atakayepatikana akiwanyanyasa wananchi hasa katika kuitisha hongo.
Mohmoud alisema kuwa visa vya unyanyasaji vimezidi kuongozeka Mombasa na kuwataka wananchi kupiga ripoti katika idara husika iwapo wamenyanyaswa, ili hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya askari jamii hao.
Aidha, aliahidi kuboresha usalama hasa sehemu za mashinani kwa kuongeza idadi ya polisi jamii.
Hatua hii inajiri baada ya naibu kamishna huyo kupokea ripoti kutoka kwa jamii kuhusiana na kunyanyaswa na askari hao hasa nyakati za usiku.