Badhii ya viongozi wanasiasa Pwani walaumu Jubilee kwa kukandamiza ugatuzi nchini.
Akizungumza siku ya Ijumaa, eneo la Kilifi, mwakilishi wa wanawake kaunti ya Mombasa Mishi Mboko alisema kuwa serikali ya kitaifa iko na njama ya kusambaratisha ugatuzi kwa kutunga sheria kiholela.
Aidha, aliongeza kuwa serikali inatumia wingi wa wabunge wa mrengo wa Jubilee katika kupitisha miswada wanayoitaka pasi kupingwa.
Mboko amepigia mfano kuwa endapo miswaada iliyoko bungeni itapitishwa kuwa sheria, basi moja kwa moja itarudisha nyuma taifa hili.
Vilevile alisisitiza kuwa kupatikana kwa katiba mpya halikuwa azimio la baadhi ya viongozi serikalini ndio maana wengi hawajalifurahia.
Wakati uo huo gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi ameilaumu serikali ya kitaifa kwa kukwamiliwa na baadhi ya majukumu ya kaunti, akisema imeleta changamoto kwa kupatikana kwa maendeleo mashinani, maendeleo ambayo mwananchi alikuwa akitegemea pakubwa ili kuimarisha uchumi mashinani.
Gavana Kingi ameitaja serikali ya Jubilee kama isiyokuwa na mapenzi na katiba mpya.