Share news tips with us here at Hivisasa

Waziri mteule wa Utalii Najib Balala ameshutumu kitendo cha majambazi kuwavamia watalii katika eneo la Watamu usiku wa kuamkia Jumapili.

Katika taarifa yake kwenye vyombo vya habari siku ya Jumapili, Balala alieleza kuwa amezungumza na mamlaka ya polisi na kaimu balozi wa Italia humu nchini na kumuhakikishia hatua za kisheria zinachukuliwa.

Balala alieleza kwamba maafisa wa polisi kote nchini wanafanya kazi kuhakikisha usalama wa wageni wote wanazuru humu nchini.

Majambazi hao waliokuwa na silaha walimuua kwa kumkatakata na mapanga mtalii mwanamke wa miaka 50 mwenye asili ya Kiitaliano.

Vile vile, wanaume wawili watalii pia walijeruhiwa katika shambulizi hilo ambapo wanapokea matibabu katika hospitli ya Tawfiq, mjini Malindi.

Kulingana na mkuu wa polisi wa kituo cha Watamu Michael Ndonga, majambazi hao walifanikiwa kuiba mali yenye thamani kubwa ikiwemo dhahabu.

Tayari washukiwa watatu wametiwa mbaroni kusaidia polisi kwa uchunguzi.