Wakaazi Molo watakiwa kujisajili kama wapiga kura Gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua amewataka wakaazi wa kaunti ndogo ya Molo wajitokeze kwa wingi na kujisajili kama wapiga kura.
Akionge mnamo Ijumaa kwenye uwanja wa Molo stadium, Kinuthia alisema idadi ambayo imejisajili kama wapiga kura ni ndogo sana. Aliwarai wakaazi wajitokeze ili wawe na nafasi na kuwachagua viongozi bora mnamo mwaka wa 2017 wakati wa uchaguzi.
Vile vile gavana huyo aliwataka wote waliojisajili kupewa vitambulisho waweze kufika katika afisi husika na kuzichukua.
Kinuthia alikuwa akitangama na wakaazi wa Molo kupitia ‘Gavana Mtaani’.