Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Zaidi ya familia mia moja katika eneo la Kosovo mjini Naivasha zimeendelea kulala nje kwenye kibaridi kikubwa kufuatia mzozo wa jamii tatu unaohusiana na ardhi.

Haya yamejiri huku usalama ukiimarishwa kwenye mipaka ya msitu wa Eburru ambapo watu watatu walijeruhiwa.

Aidha hali ya wasiwasi imeendelea kuenea eneo hilo ambalo limekuwa likikumbwa na mizozo ya ardhi.

Mkuu wa wilaya ya Naivasha Abraham Kemboi aalisema kuwa kamati ya usalama ilikuwa imefanya mikutano ya Amani huku polisi zaidi wakitumwa eneo hilo kuimarisha usalama.

Akizungumza afisini mwake, Kemboi alisema kuwa kamati ya watu kumi kutoka jamii hizo tatu imebuniwa ili kuangazia maswala tata yanayoadhiri jamii hizo.