Gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua amewahakikishia wakaazi wanaoishi na changamoto ya ulemavu kwamba haki zao zitazingatiwa.
Akizungumza siku ya Jumamosi wakati alipoongoza hafla ya kupeana vifaa vya matumizi kwa walemavu katika ukumbi wa Menengai, Gavana Mbugua alisema kuwa maslahi ya walemavu wote yatazingatiwa.
"Kaunti ya Nakuru tuko kipaumbele kuhakikisha kwamba wanaoishi na changamoto ya ulemavu wanapata misaada" Mbugua alisema.
Wakati huo huo ametoa wito kwa bunge la kaunti ya Nakuru kuhakikisha kwamba sheria za walemavu zinazingatiwa.
"Ningeomba bunge la kaunti ya Nakuru kubuni sheria muhimu za kuwasaidia walemavu"Mbugua aliongeza.