Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana wa kaunti ya Nakuru Kinuthia Mbugua ameitaka wizara ya fedha kutengea pesa zaidi kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC) ili iweze kuwasajili wapiga kura.

Mbugua alisema ukosefu wa fedha za kutosha umeathiri pakubwa shuguli za IEBC na kuitaka serikali kutenga fedha zaidi katika bajeti ijayo.

"IEBC inafanya kazi nzuri lakini changamoto kubwa kwao ni ukosefu wa fedha na ningetoa wito kwa serikali kuipa tume hiyo fedha zaidi ili kufanikisha shuguli zake," Kinuthia alisema.