Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Aslimia 70 ya viongozi wa kaunti ya Nakuru katika nyanja mbali mbali ikiwemo bunge,  wameonekana kujikakamua kutekeleza wajibu wao kwa mwananchi huku aslimia 30 wakikosa kuwajibika.

Mwenyekiti wa chama cha TNA Nakuru Samuel Githaiga alisema kuwa baadhi ya viongozi wamefeli katika majukumu yao kimaksudi kwa kujali tu maslahi yao pasi na kujali mwananchi wa kawaida.

Bila kutaja majina alisema: “Kwa kadri wengi wao wamefanya kazi, pengine aslimia sabini hivi.lakini bado kuna wale ambao kazi yao ni kuongea tu na hatuoni wanachokifanya.” 

Na huku uchaguzi mkuu wa 2017 ukikaribia, Githaiga alitoa wito kwa wakaazi wa kaunti ya Nakuru kuwapiga msasa viongozi na utendakazi wao kabla ya kuwapigia kura.

“Wakaazi wa Nakuru wawe watulivu kama vile tulichaguana kwa utulivu 2013. Hatutaki vita, na kwa hivyo tukiingia katika uchaguzi ujao tuwe watulivu ili kazi za kila mmoja zipate kuendelea baada ya uchaguzi,” Githaiga alisema.