Share news tips with us here at Hivisasa

Baada ya kuzinduliwa rasmi maktaba maalumu katika eneo la Majengo kaunti ya Mombasa, maktaba hiyo imepewa jina la hayati Profesa Ali Mazrui kama kumbukumbu ya msomi huyo na balozi rasmi wa Marekani Robert Godek ambaye alisimamia shughuli hiyo.

Kwenye mahojiano na waandishi wa habari jijini Mombasa Balozi huyo Robert Godek, amesema kuwa maktaba hiyo imefanya uamuzi huo mahusus ili kuweza kumpa heshima hayati Mazrui ambaye alisema mchango wake katika masuala ya elimu katika ulimwengu wa fasili na kupigania haki za mtoto wa kiafrika kupata elimu kupitia vitabu vyake.

Godek amesema kuwa wataendelea kutoa msaada kwa watoto wa Kenya ambao wana ari na moyo wa kusoma na serikali yake inatarajia kuanzisha vituo zaidi vya maktaba vya American Corner ambavyo dhamira yao ni kuwapa nafasi raia wa nchi ya Kenya.

Hii itakuwa wakfu wa kwanza kumtambua wiji huyo ambaye alikuwa amefahamika kwa kuandika vita kwenye mfumo wa kuigiza kama vile kitabu chake maarufu Kilio Cha Haki ambacho kiliweza kuigizwa na shule nyingi pamoja na mashirika ya kutoa filamu nchi na kote ulimwenguni kuonyesha hali ya mtoto wa Kiafrika.

Balozi huyo yuko katika ziara ya eneo la Pwani kwa masuala ya utalii pamoja na kukutana na viongozi wa kaunti hiyo ya Mombasa kwenye miradi mbalimbali.