Wakaazi wa mtaa wa Rhonda viungani mwa mji wa Nakuru wameitaka serikali ya kaunti ya Nakuru kuachilia pesa zilizotengwa kukabiliana na maafa ya mvua ya El~Nino.
Wanasema pesa hizo zitawasaidia waliopoteza makazi yao kutokana na mafuriko.
Wakaazi hao ambao nyumba zao zilisombwa na mafuriko wansema kuwa hawajapata usaidizi wowote kutoka kwa serikali licha ya kuahidiwa.
Wakiongozwa na Andrew Kimotho ambaye ni mzee wa kijiji amesema kuwa watu wengi waliohama nyumba zao baada ya mafuriko kutokea wangali wanakaa kwenye kambi za muda na mashule katika eneo hilo.
Kimotho amesema kuwa wengi wa waathiriwa wameshindwa kutafuta nyumba mpya kwa kuwa hawana fedha zozote.
“Serikali ilituahidi kuwa pesa zaelnino zitatusaidia na tunajua kuna pesa ilitengwa kufanya kazi hiyo lakini hadi kufikia sasa sisi bado hatujaona afisa wa serikali akija hapa kutuona tangu nyumba zetu zija maji ya mafuriko,” aksema Kimotho.
“Tunamuomba Gavana Kinuthia Mbugua aje atutembelee na atusaidie kupata makaazi mengine kwa sababu kuan watu wako na watoto wadogo hapa na hali yao inazidi kuzorota,” akasema.
Stella Mwelu ambaye aliiathriwa na mafuriko hayo aesea kuwa amelazimika kutafuta makazi ya muda katika shule jirani huku akisuburia usaidizi kutoka kwa serikali ya kaunti.
“Tuliambiwa pesa itakuja na bado tunasubiri lakini serikali inakawia sana na tungeiomba iharakishe ili tuweze kupata makazi mazuri kwa ajali ya watoto wetu,” akasema Mwelu.
Mtaa wa Rhonda ni kati ya mita iliathirika pakubwa a mvua ya El~Nino ambayo inanyesha maeneo mengi nchini.