Maafisa wa afya ya umma mjini Nakuru Jumatatu walinasa zaidi ya kilo 200 ya nyama ambayo haijakaguliwa ikishukishwa katika duka moja la nyama mjini Nakuru.
Aidha ilibainika kuwa nyama hiyo ilikuwa imesafirishwa kutoka eneo la Elburgon jimbo ndogo la Molo .
Kulinganana afisaa mkuu wa afya ya umma katika jimbo la Nakuru Samwel Kingori ni kuwa visa viwili vilikuwa vimeripotiwa mapema mwezi jana kuhusu wahusika katika uuzaji wa nyama ambayo haijakaguliwa kisa anachodai afisi yake ilikuwa ikichunguza .
Aidha ametaja kushangazwa na kisa cha leo akihoji kuwa wafanyibiashara wa tukio la leo walikuwa tayari na stakabadhi rasmi za kusafirisha vyakula (Food Transport Certificate) akihoji kuwa afisi yake inachunguza kubaini zilikotolewa stakabadhi hizo.
Amesema kuwa afisi yake itatekelweza sharia kali ili kuwanasa watu wanaosafirisha nyama ambayo haijakaguliwa.
“Afisi yangu inaunda sera zitakazoongoza maswala yote ya nyama na zitazohakikisha kuwa magari yote ya usafiri wa bidhaa za nyama yamepewa leseni sawia na maandishi yake spesheli pamoja na wahudumu wake kuwa na stakabadhi za kiafya na hata nguo rasmi kwa kazi zao,” Kingori alisema.