Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC tawi la Central Rift imetoa wito kwa wanasiasa kuunganisha taifa.
Mratibu wa IEBC kanda ya Central Rift David Towett amesema kuwa wanasiasa wana fursa nzuri ya kuwaunganisha wakenya, na bali si kuwaganywa kwa misingi ya kikabila.
"Ningependa kuwarai wanasiasa, tafadhali huu ndio wakati wa kuwaunganisha wananchi kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao," alissema Towett.
Wakati huo huo, afisa huyo wa IEBC amewapongeza viongozi wa kidini kwa kuzidi kueneza habari muhimu za usajili wa wapiga kura.
Amesema kuwa katika kukamilika kwa shughuli hiyo, anatumai wengi wa wakazi watakuwa wamejisajili kama wapiga kura.