Mbunge wa zamani wa Subukia Koigi wa Wamwere, amewataka wakenya kuishi maisha ya unyenyekevu, yasiyo ya kujitakia utajiri mwingi, mali kupita kiasi na mashamba, sawa na alivyofanya Yesu kuzaliwa katika maisha ya uchochole.
Mwandishi huyo wa vitabu na mchanganuzi wa maswala ya kisiasa, alisema ni kinaya walimwengu kujifanya wanasherehekea siku ya kuzaliwa Yesu, wakati wengine wanaishi maisha ya anasa na yaliyojaa ufisadi.
Akiongea na mwandishi huyu mjini Nakuru, Koigi ametaka viongozi nchini kuiga mfano wa Yesu na kuhakikisha wafuasi wao wana chakula cha kutosha, wamekomesha ufisadi pamoja na umaskini..
“Yesu aliwashibisha wote waliomfuata. Hapa nchini Kenya tuliowachagua, wanastahili kuiga mfano huo. Wao ni kama yesu wetu, ambao ni lazima wapme maskini kazi aweze kujipatia chakula,” Koigi alisema.
“Hata hivyo Koigi amesifia ujasiri wa waislamu waaliokinga wakenya wenzao ambao ni wakristu, dhidi ya kushambuliwa na magaidi wa Al-shabab,” aliongeza.