Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Ufisadi unachukua mwelekeo hatari kadri tunavyokaribia uchaguzi mkuu 2017, jaji mkuu (CJ) Willy Mutunga ametahadharisha.

Mutunga alikuwa mjini Naivasha katika hoteli ya Enashipai Spa Alhamisi wakati wa kongamano la baraza la pili kuhusu utawala wa sheria na baraza la magavana.

Akitoa mfano wa ufisadi wa pesa za umma nchini, Mutunga aliwarai walio mamlakani kuchunguza kwa undani visa vya ufisadi akisema utakuwa na madhara makubwa kwenye chaguzi hizo.

Mwenyekiti wa baraza la magavana nchini (COG) Peter Munya alipongeza idara ya mahakama kwa kutetea vigezo vya ugatuzi.

Kati ya sakata fisadi za hivi maajuzi ambazo zimegonga vichwa vya habari nchini Kenya, ni kupotea kwa shilingi milioni 791 katika wizara ya ugatuzi, milioni 180 katika hazina ya vijana YEDF, pamoja na sakata ya Chikengate inayozunguka baadhi ya maafisa waliokuwa wanaongoza tume ya IEBC.