Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Jumuiya ya Ulaya kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa imeanzisha mpango wa lishe bora kwa akina mama na watoto, ili kukabiliana na maradhi ya utapia mlo katika eneo la Pwani.

Haya yanaarifiwa huku takwimu zikionyesha kuwa wanawake 650 kati ya laki moja wanaojifungia hufariki kutokana na ukosefu wa lishe bora, huku watoto 118 kati ya watoto elfu moja wakifariki kutokana na utapia mlo.

Akiongea baada ya uzinduzi wa mpango huo katika eneo la Samburu, Waziri wa Afya kaunti ya Kwale Dkt Athman Chiguzo, alisema kuwa maafa yameongezeka kutokana na akina mama kupuuza maagizo wanayopewa kuhusu lishe bora.

Dkt Chiguzo ameeleza kuwa Serikali ya kaunti eneo la Pwani zifaa kuipa kipaumbele sekta ya afya, ili kuhakikisha kuwa wakaazi wanapata huduma bora hususan akina mama waja wazito wakati wa kujifungua.

“Tunaziomba serikali za ugatuzi katika eneo letu la Pwani kuhakikisha kuwa zichukua jukumu muhimu hasa sekta ya afya wanaipa kipao mbele kuhakikisha kuwa masuala ya afya yanaangaziwa,” alisema Chiguzo siku ya Ijumaa katika hafla ya kuzinduo mango huo.

Kwa upande wake Hjordis Ogendo aliye Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya alisema kuwa watoto elfu 140, na akina mama elfu 30 watafaidishwa na mpango huo utakaoendelezwa kwa muda wa miaka miwili.

Naye mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Ann Robin aliitaka jamii izingatie malezi na lishe bora huku mpango huo ukitarajiwa kunufaisha jumla ya kaunti 9.