Share news tips with us here at Hivisasa

Takriban wanafunzi 100 kutoka jamii ya Maasai katika eneo bunge la Taveta wamelazimika kukatiza masomo yao baada ya wazazi wao kuwatoa shuleni ili kuchunga mifugo.

Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumamosi, Mwakilishi wa Wadi ya Mata eneo bunge la Taveta Reuben Kipampi alisema kwamba hatua hiyo imetokana na idadi kubwa ya jamii hiyo kukosa misingi bora ya elimu.

Kipampi alizishiniza idara husika kuingilia kati swala hilo na wahusika kukamtwa kwa kuwanyima haki zao watoto hao ya kielimu.

“Tunaitaka idara husika hususan ile ya elimu na zile za watoto kuingilia kati swala hilo na kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya jamii hiyo ya Wamaasai kwa kukiuka haki za watoto na kuwanyima elimu," alisema Kipampi.

Amedai kuwa maafisa husika wamekuwa wakishiriki hongo na kusalia kimya na akaita tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi kuingilia kati na kuchunguza kisa hicho.