Share news tips with us here at Hivisasa

Kahawa chungu au thungu, kama inavyotambulika kwetu Mombasani imekuwa maarufu toka enzi za akina yakhe, na bado hata vijana wa sasa wanaikumbatia vilevile.

Kinywaji hiki hunywewa jioni wakati wa mapumziko.

Wengi wa wakaazi hujiuliza kinywaji hiki hutengezwa vipi? usijali utamakinika. Tupike ya watu wawili kwanza.

Viungo

• Maji vikombe 4

• Kahawa vijiko 2

• Tangawizi kijiko 1

• Poda ya Cinnamon kijiko 1/4

• Iliki iliyosagwa kijiko 1/4

• Karafuu nzima vipande 2

• Kongomanga kiasi

Maandalizi

• Changanya viungo vyote kwenye sufuria na uongeze maji.

• Bandika kwenye jiko la moto na upike kwa dakika 13.

• Punguza moto na upike kwa takriban dakika 3 kisha uepue na kutia ndani ya chupa.

usije ukasahau ukatia sukari! Chungu ndio tamu.

Waeza kunywa na vishete, mlenge au mitahi, vile utakavyopenda.

'Waraibu' wa kinywaji hiki husema njugu hufanya 'maajabu' unapoambatisha na kahawa thungu.