Mwenda zake Ahmed Darwesh, aliyekuwa mwanahabari wa kituo kimoja cha runinga hapa nchini, alizikwa katika makaburi ya Kikoani siku ya Jumanne jioni.
Mwili wa mwenda zake ulisafirishwa hadi Mombasa kwa maziko siku ya Jumanne, huku ndege iliyoubeba ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Moi Mombasa muda mfupi baada ya saa tano asubuhi.
Swala maaluum kwa Ahmed ilifanyika katika msikiti wa Memon kabla ya shunghuli ya maziko katika makaburi ya Kikowani.
Ahmed alidhibitishwa kufariki katika hospitali ya Mater jijini Nairobi kutokana na kile kilichotajwa kama ugonjwa wa kisukari.
“Naam, Mtazamaji kufikia hapo sina la ziada hila kuhitimisha taarafika za KTN leo wikendi, Maulana akiridhiria hapo kesho basi tutakutana tena papa hapa inshalah..” ndivyo alivyomaliza kusoma taarifa za saa moja jioni siku ya Jumapili na iliyokuwa mara yake ya mwisho kwenda hewani.
Mazishi yake Darwesh yalihurudhiwa na wanahabari mashuhuri nchini huku Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho na mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir wakiwaongoza maelfu ya waombozaji katika mzishi hayo.
“Tumehuzunishwa sana na kifo cha ndungu na rafiki wetu Darwesh. Mombasa yote pamoja na serikali ya kaunti ya Mombasa inajiunga kusema pole kwa familia ya mwenda zake,” Joho alisema akiwahutubia waombolezaji.