Share news tips with us here at Hivisasa

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ameitaka serikali kuu kuipa mamlaka zaidi tume ya ardhi nchini NLC ili iweze kushughulikia vilivyo maswala ya ardhi.

Kalonzo alisema kuwa tume hiyo ina umuhimu mkubwa zaidi katika kushughulikia maswala ya ardhi katika nchi hii lakini akaongeza kuwa imekosa kupewa huru wa kutekeleza majukumu yake.

Akiongea huko Likoni siku ya Jumapili, Kalonzo alisema kuwa tume hiyo imeshindwa kusuluisha changamoto ya ardhi ukanda wa pwani kutokana na serikali kuingilia shughuli zake na hivyo kukosa nguvu dhabiti.

“Unyanyasi mkubwa hapa Kenya unapitia katika ardhi, na tunataka tume ya ardhi inayoongozwa na Mohamed Swaruzi ipewe mamlaka zaidi ili ili iweze kutatua mambo haya,” Kalonzo alisema.

Kiongozi huyo wa Cord pia aliwahimiza wakaazi wa pwani kusimama kidete na kutetea haki yao kuhusu mashamba akisema kuwa watu wenye mamlaka ya juu huchukua fursa hiyo na kuingilia mashamba ya wapwani.

“Tume hiyo ikipewa nguvu itahakikisha kwamba hakuna mtu anayetoka eneo lingine na kuja kuwanyanyasa na make mkijua kwamba ardhi ya pwani ni ya watu wa pwani,” Kalonzo aliongeza.

Wakati huo huo Kalonzo alikosoa ziara ndefu ya rais Uhuru Kenyatta eneo la Pwani mapema mwaka huu akiitaja kama isiyokuwa na faida yoyote kwa wapwani.

Kuhusu shamba la Waitiki, Kalonzo aliirai serikali ya kaunti ya Mombasa kujitolea na kusaidi maskwota wa shamba hilo kulipa pesa walizotozwa na serikali kuu.