Mweka hazina wa chama cha Kenya National Union of Teachers (Knut) tawi la Masaba Kusini Evans Kalulu anataka eneo hilo kujivunia waziri wa elimu Fred Matiang'i.
Bonuke ameitaka jamii ya Abagusii kwa jumla kufurahia na kutumia wadhifa huo vizuri ili kurejesha viwango vya elimu eneo hilo viliyokuwa awali.
"Kisii imekua katika mstari wa mbele kielimu kwa miaka kadhaa. Sasa ni wakati wa kung'ara kielimu kote nchini na kutupilia mbali ule uzembe tumekuwa nao pale ambapo viwango vyetu vya elimu vilididimia," Kalulu alisema.
Wakaazi wa eneo la Kisii aidha wamepongeza Raisi Uhuru Kenyatta kwa wizara hiyo wakisema elimu ndio nguzo ya taifa na sasa ni wakati wa jamii hiyo kuimarisha masomo na kurejesha umaarufu wa Abagusii.
Akihutubia umati, aliyekuwa kamishina wa uchaguzi Hezekiel Machogu pia amepongeza serikali kwa juhudi zake ingawa changamoto tele serikalini.
"Sisi kama wananchi wa taifa la Kenya ni lazima tujaribu kusaidia viongozi wa serikali yetu kufanikiza miradi na maendeleo yake kwa huduma bora kwetu la sivyo sisi ndio tutaumi," Machogu alisema.
Wakaazi hao sasa wanataka ushirika wa wahusika hili kuimarisha masomo katika kaunti hiyo na viunga zake.