Kamishna wa kaunti ya Nyamira Josphine Onunga amewaonya vikali machifu na manaibu wao wanaoruhusu ugemaji wa pombe katika maeneo yao ya utawala.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kwenye kikao na wanahabari afisini mwake, Onunga alisema kuwa afisa yeyote wa utawala atakaye patikana akiruhusu ugema kuendelea atachukuliwa hatua kali za kinidhamu.

"Ugemaji na ubugiaji wa pombe haramu ni hatia katika sheria za taifa hili na ndio maana nawaonya vikali machifu na manaibu wao watakaopatikana wakiruhusu utovu huo watachukuliwa hatua kali zakinidhamu," alisema Onunga.

Onunga aidha aliongeza kwa kuwaonya vikali watu wanaoajiri watoto ili kufanya kazi za sulubu huku akisema kuwa watoto wana haki ya kupata masomo.

"Kuna ripoti zinazonifikia kwamba kuna watu wanaoajiri watoto ili kuwafanyia kazi za nyumbani ila wacha wajue kwamba ajira kwa watoto ni kinyume cha sheria na yeyote atakayepatikana atakabiliwa kisheria." aliongezea Onunga.