Wakaazi wa mtaa wa Kibera wamehimizwa kukumbatia umuhimu wa usafi wa meno.
Haya ni kwa mujibu wa maajenti wa kampuni ya Unilever walipokuwa kwenye tamasha za kutafuta talanta miongoni mwa vijana katika uwanja wa Kamukunji, Kibera siku ya Jumamosi.
Kampuni hiyo ambayo ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa tamasha hizo imetoa dawa ya meno aina ya Closeup na hata kuwaonyesha wakaazi jinsi ya kupiga mswaki.
Wakazi wengi ambao walihudhuria tamasha hiyo walipongeza kampuni ya Unilever kwa kuwapa dawa ya Closeup bure.