Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Waziri wa barabara wa kaunti ya Nakuru Joel Maina Kairu ameitetea serikali ya kaunti ya Nakuru ya kwamba haikula pesa zilizokuwa zimekusudia kuwasaidia waathiriwa wa elnino.

Akizungumza mjini Nakuru, Waziri kairu aliweka bayana kwamba serikali ya kitaifa ilikuwa imeahidi kuipa kaunti ya Nakuru shilingi milioni mia tano, kwa ajili ya kujitayarisha na kukabiliana na athari za mvua ya elnino, jambo ambalo serikali ya kitaifa haikutekeleza.

Matamshi haya yanajiri miezi michache baadaya kaunti ya Nakuru kushutumiwa kula pesa za waathiriwa wa elnino, baada ya gavana wa kaunti hiyo Kinuthia Mbugua kutangaza kubuniwa kwa kamati ya kusimamia swala hilo  mwezi Oktoba mwaka jana.