Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya Kaunti ya Kisii imeombwa kujenga chuo cha kukuza talanta katika kaunti hiyo ili kukuza vipaji vya vijana na kuwawezesha kujiendeleza kimaisha.

Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatono mjini Kisii, mwenyekiti wa maktaba nchini Samuel Nyangeso, alisema kuwa hatua hiyo itawasaidia vijana kukuza vipaji vyao na kujiendeleza katika maisha kupitia talanta hizo.

Nyangeso alisema kuwa kuna haja ya kutumia pesa ambazo hutengwa na serikali kwa sekta ya michezo, kufanya miradi mbalimbali , ujenzi wa chuo cha kukuza talanta ukiwa moja wapo ya miradi hiyo.

“Naomba serikali ya kaunti kujenga chuo cha kukuza talanta katika kaunti yetu ili tuweze kukuza vipaji vya vijana,” alisema Nyangeso.

Aliongeza, “Kuna vijana wengi katika kaunti yetu walio na vipaji mbalimbali lakini kile wanachokosa ni uungwaji mkono na njia ya kukuza talanta zao.”

Aidha, aliomba viongozi kushirikiana kuhakikisha vipaji vya vijana vinakuzwa kwani idadi kubwa ya vijana hawana uwezo wa kujiendeleza.