Share news tips with us here at Hivisasa

Serikali ya kaunti ya Nyamira imeombwa kuwaongezea wafanyibiashara wanaouza bidhaa zao katika kituo cha magari mjini Nyamira muda zaidi ili kuhamia sehemu nyingine.

Hii ni baada ya serikali hiyo kutangaza kuwa wafanyibiashara wote walioko katika kituo hicho cha magari mjini Nyamira wahame mara moja ili kuruhusu ukarabati wa kituo hicho kufanywa, jambo ambalo limepingwa vikali kupitia viongozi pamoja na wakazi.

Akizungumza jumatatu na mwandishi huyu mwakilishi wa wadi ya Nyamira Township Robert Ogwaro alisema ikiwa serikali inahitaji kukarabati kituo cha magari, sharti ijali maslahi ya wafanyibiashara kwani hutafuta riziki kwa kuwapa muda wa miezi mitatu ili kutafuta mahali pa kufanyia shughuli zao kuliko kuwafurusha kwa siku moja.

“Naiomba serikali ya kaunti ya Nyamira kuongezea wafanyibiashara wetu muda zaidi ili watafute mahali pa kufanyia biashara zao,” alisema Ogwaro.

Aidha, mwakilishi huyo aliiomba serikali ya kaunti kutimiza ahadi iliyotoa kwa kujenga vibanda vya mabati katika kituo hicho ili wafanyibiashara kukodi kwa kazi zao.

“Naiomba serikali kuegeza vibanda vya mabati mjini Nyamira kila sehemu jinsi ilivyoahidi hapo mbeleni ili wafanyibiashara kupata mahali pa kufanyia biashara zao,” aliongeza Ogwaro.

Sasa jukumu ni la serikali ya kaunti ya Nyamira kuitia wito wa mwakilishi ili kuonyesha usawa na haki kwa wafanyibiashara.