Serikali ya kaunti ya Kisii imeombwa kuunganisha nguvu za umeme katika hospitali ya Ogembo level 5 ili kuimarisha huduma bora za matibabu katika hospitali hiyo.
Ombi hilo limetolewa baada ya kubainika kuwa nguvu za umeme zilioko katika hospitali hiyo hazina nguvu ambazo hospitali kubwa kama hiyo inastahili kuwa nayo na kuhitaji nguvu za umeme za '3 phases' ili kuimarisha huduma bora za matibabu kwani kuna mashine ambazo huhitaji kutumia nguvu za umeme za juu.
Akizungumza siku ya Jumanne katika sherehe ya mazishi iliyoandaliwa katika eneo la Bisiongororo wadi ya Boochi mhudumu wa afya katika hospitali hiyo Dickson Monari alisema hospitali ya Ogembo inahitaji kuunganishiwa umeme wa '3 phases' ili kutoa huduma bora iliyo kamilifu.
Kulingana naye stima iliyoko kwa sasa haitoshereshi kutoa huduma kwani kuna mashine ambazo huhitaji nguvu za umeme za juu na kushindwa cha kufanya jambo ambalo limewapelekea kuomba serikali ya kauti kuingilia kati kutoa msaada huo.
“Katika hospitali yetu ya Ogembo hatuna stima ya kutosha na kuna haja ya kuunganishiwa stima ya '3 phases' na serikali ya kaunti ya Kisii kwani sekta ya afya iko chini ya uongozi wa kaunti,” alisema Dickson Monari mhudumu wa afya katika hospitali ya Ogembo.