Wanakandarasi katika kaunti za Kisii na Nyamira wameomba serikali ya kaunti ya Kisii kuwalipa pesa zao kwa wakati unaofaa baada ya kuzimaliza kandarasi zao ambazo wanakabidhiwa na serikali hiyo.
Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumanne mjini Kisii wanakandarasi hao chini ya mwavuli wao [Kisii, Nyamira contractors association] wakiongozwa na katibu wao Evans Ombaso walilaumu serikali ya kaunti ya Kisii kwa kuchelewa kuwalipa pesa zao kwa wakati unaofaa baada ya kuzimaliza kandarasi na kuomba kulipwa pesa zao kwa wakati unaofaa.
Kulingana nao hadi sasa serikali ya kaunti hiyo haijawalipa millioni 200 ambazo wanaendelea kuzifuatilia huku naibu gavana wa kaunti hiyo Joash Maangi kuwahidi kulipwa pesa zao walizozifuatilia hapo awali jambo ambalo hawajatimiziwa.
“Hatufurahi tunapochelewa kupewa pesa zetu baada ya kazi, maana huwa tunakopa pesanna baada ya kazi tunaambiwa tusubiri ,tutasubiri hadi wakati upi? Sasa hivi serikali ya kaunti ya Kisii haijatulipa pesa zetu ambazo ni shiilingi millini 200 na tumeambiwa tusubiri,” alisema Ombaso.
“Tunaomba kulipwa pesa zetu kwa muda unaofaa na wasiwe wanachelewesha pesa kila wakati,” aliongeza Ombaso.
Aidha, waliomba tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC kuchunguza serikali ya kaunti hiyo kubaini chanzo cha kuchelewesha kulipa wanakandarasi pesa zao baada ya kazi.
Matamshi hayo yaliungwa mkono na mwenyekiti wa chama hicho cha wanakandarasi Jackson Onkubo ambaye alisema wawe wanalipwa pesa zao kwa wakati ufaao.