Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Serikali ya Marekani imeahidi kushirikiana na Kenya katika kuimarisha juhudii za kukabiliana na uwindaji haramu pamoja na usafirishaji wa pembe za ndovu na kifaru katika mataifa mbalimbali kupitia Bandari ya Mombasa.

Waziri wa Usalama wa ndani wa Marekeni Bi Sally Jewell alisema kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza kuangamizwa kwa wanyama pori sambamba na kuzuia kuenea kwa biashara hiyo haramu hadi mataifa ya Vietnam, Uchina, Thailand, Malaysia, Ufilipino, Uganda na Tanzinia.

Akiongea na wanahabari baada ya kukutana na Viongozi wa kuu wa Halmashauri ya Bandari nchini KPA pamoja na Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho katika bandari ya Mombasa siku ya Jumanne, Waziri Jewell amesema kuwa serikali ya Marekani itazidisha juhuzi hizo ili kuona kwamba wahusika wanakamatwa na kuimarisha usalama wa wanyamapori pamoja na kueneza utamaduni wa afrika.

"Serikali ya Marekani na Kenya zimekubaliana kushirikiana kukabiliana na biashara haramu ikiwemo uwindaji haramu na usafirishaji wa pembe za ndovu na kifaru kupitia bandari ya Mombasa ili kuona kwamba utamaduni wa afrika unazingatia na usalama wa wanyama pori," alisema Jewell.

Kwa upande wake Waziri wa Mazingira na rasilimali za umma nchini Bi Judy Wakhungu alisema kuwa serikali ya Kenya inaunga mkono juhudi hizo kwani idadi ya wanyama pori waliyokuwa wakiangamizwa tangu mwaka wa 2012 imepungua kwa kiasi kibwa kufikia sasa.

Alisema kuwa lazima usalama wa wanyamapori kuzingatiwa kwani ni kivutio cha utalii nchini na akasema kuwa maafisa wa muungano wa Halmashauri nchini zinazohusika kukagua makasha bandarini humo zitahakikisha kuwa ukaguzi huo unafanywa na maumbwa yaliyofunzwa kiusalama ili kunasa biashara zote haramu.

Hafla hiyo ya kuonyesha jinsi makasha yatakavyokaguliwa kabla ya kusafirishwa nchini zingine imeshuhudiwa na Balozi wa Marekani humu nchini Robert Godec, Katibu wa Wizara ya mazingira nchini Margaret Mwakina, Katibu katika Wizara ya uchukuzi Irungu Nyakera, Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho, Mkurugenzi wa KPA Gichuri Ndua, Naibu Kamishna wa KRA Nicholas Kinoti pamoja na viongozi wengine serikalini.