Mshukiwa wa mauaji ya makahaba mjini Nakuru Anthony Wachira Mukuria, Jumatatu alifikishwa katika mahakma moja ya Nakuru.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshukiwa alifikishwa mbele ya jaji Maureen Odero, akishtakiwa kuhusika na mauaji ya mfanyibiashara ya ngono Maureen Wanjiru mnamo Januari 17, 2016, katika eneo la Freehold viungani mwa mji wa Nakuru.

Hata hivyo mshukiwa hakujibu wala kukubali mashtaka dhidi yake, kwani mahakama ilielekeza ripoti ya uchunguzi wa kiakili dhidi yake itolewe mahakamani kabla ya kupewa nafasi ya kujibu mashtaka.

Kesi hiyo sasa itasikilizwa tarehe mosi mwezi Februari.