Kesi inayowakabili wanachama wa kundi liloharamishwa la 'Mombasa Republican Council' MRC iliyopangwa kusikizwa siku ya Jumatatu imeahirishwa hadi ya siku ya Jumanne.
Akitoa uamuzi huo, Hakimu mkazi wa Mombasa Paul Mutai, alisema kesi hiyo imeahirishwa kutokana na ombi la wakili anayewakilisha kundi hilo, kuomba ruhusa kwa kusema kuwa ana majukumu mengine katika mahakama ya Malindi.
Jumla ya wanachama 42 wa kundi la MRC walitiwa mbaroni katika eneo la Tiwi, mjini Mombasa, siku ya Ijumaa kwa madai ya kukongamana kinyume cha sheria kwa agenda isiyo julikana.
Kesi hiyo sasa imeratibiwa kusikizwa siku ya Jumanne, Januari 5, 2016.