Mwenyekiti wa Grassroot Women Empowerment Grace Kibuku amewashtumu vikali viongozi fisadi na wanaoendeleza ukabila.
Kibuku anasema kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba hata baada ya kuchaguliwa, viongozi wameendeleza ukabila na kupelekea akina mama na makundi yaliyosahaulika kubaki nyuma.
"Nashangaa kwamba viongozi wetu wanaendeleza ukabila hata katika afisi za umma badala ya kuwahudumia wananchi," alisema Kibuku.
Kiongozi huyo ambaye pia ni balozi wa amani humu nchini ametoa wito kwa wanasiasa kuchunga matamshi yao tunapoelekea uchaguzi mkuu.