Kijana mwenye umri wa makamo ameachiliwa kwa faini ya shilingi 5,000 kwa shtaka la kuiba keki.
Mshtakiwa, Rajab Omar, anadaiwa kuiba paketi nane za keki katika duka moja kwenye eneo la Majengo mnamo Machi 1, 2016.
Omar aliiambia mahakama siku ya Jumatano kuwa alikuwa anahisi njaa ya haki ya juu ndiposa ikamlazimu kuiba cake hizo ili kukidhi mahitaji yake.
Hakimu katika mahakama ya Mombasa Diana Mochache alimuachilia kwa faini ya shilingi 5,000 na kumuonya kutoiba tena.