Kijana wa umri wa makamo amefunguliwa mashtaka ya kujaribu kujinyonga.
Mahakama ilielezwa siku ya Jumatano kuwa mshtakiwa, Samuel Makokha anadaiwa kujaribu kujinyonga kwa kutumia nyaya ya nguvu za umeme mnamo Machi 8, 2016, katika eneo la Mtongwe.
Makokha alikubali shtaka hilo mbele ya Hakimu Diana Mochache na kusema kuwa aliamua kuchukuwa hatua hiyo baada ya kukosa ulezi bora na mapenzi ya wazazi.
Mahakama iliagiza mshukiwa huyo kufanyiwa uchunguzi wa akili kabla kuhukumiwa kwa kosa hilo.
Kesi hiyo itatajwa tarehe Machi 22, 2016, baada ya uchunguzi kufanywa.