Kijana mmoja amehukumiwa kifo katika mahakama ya Mombasa baada ya kupatikana na makosa ya wizi wa mabavu na mauaji ya polisi.
Mahakama ilielezwa kuwa mnamo Disemba 18, 2011, mshitakiwa Shem Odero, na wenziwe wakiwa wamejiahami kwa mapanga na visu, walimvamia John Kamau ambaye alikuwa polisi na kumua katika eneo la Majengo Mapya huko Likoni.
Vilevile kwenye uvamizi huo, Odero na wenzake walimpokonya askari huyo bunduki yake aina ya AK47 yenye thamani ya Sh46,000.
Akitoa hukumu hiyo siku ya Jumanne, Hakimu mkuu wa mahakama ya Mombasa Susan Shitub alisema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa ni wazi kuwa Odero alihusika pakubwa katika uahalifu huo.
Aidha, alisema kuwa hukumu hiyo itakuwa funzo kwa wengine wanaojihusisha na wizi wa mabavu na mauwaji ya kiholelaholea.