Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kijana mwenye umri wa makamo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani na Mahakama moja ya Mombasa, kwa kosa la kuiba simu ya rununu.

Upande wa mashtaka ulielezea Mahakama kuwa Mnamo Januari 17, 2016 katika eneo la Consolata huko Likoni, mshatkiwa, Juma Saidi, anadaiwa kuiba simu ya rununu yenye thamani ya shilingi elfu tisa, mali ya Jane Muthoni.

Katika mahakama hiyo hiyo, mshukiwa mwingine Hussein Adan, alifungwa miaka miwili gerezani kwa kosa la ulaghai wa shilingi 3,300 kutoka kwa mlalamishi, Fredrick Iyende.

Adan anadaiwa kutekeleza kosa hilo mnamo Desemba 30, 2016.

Vijana hao wako na siku 14 za kakata rufaa kupinga uamuzi huo.