Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kijana wa umri wa makamo alifikishwa mahakamani kujibu shtaka la kupatikana na kisu katika jengo la Mahakama ya Mombasa.

Upande wa mashtaka ulieleza mahakama siku ya Jumanne kuwa mshtakiwa, Jacob Odour anadaiwa kupatikana na kisu hicho katika jengo la Mahakama ya Mombasa alipohudhuria kikao cha kesi nyingine inayomkabili siku ya Jumatatu.

Odour alikanusha madai hayo mbele ya Hakimu Samuel Rotich.

“Sikuwa na kisu bali nimesingiziwa na mwendesha mashtaka baada ya kukiuka agizo lake la kutoa hongo,” alisema Oduor.

Hakimu Rotich alimtoza dhamana ya shilingi elfu 50.

Kesi hiyo itasikilizwa Januari 24, 2016.