Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kijana mmoja kutoka eneo la Industrial, Naivasaha amejitia kitanzi katika hali tatanishi.

Tukio hilo la Jumapili mchana limewaacha wakazi na butwaa wasijue la kusema, huku wakithibitisha kuwa alikuwa mzima wa afya.

"Alikuwa katika hali nzuri Jumamosi lakini hatujui in shetani mgani huyu alimwingia na akaamua kujitoa uhai," alisema Simon arunda ambaye ni jirani wa marehemu. 

Ni matamshi sawia yaliyotolewa na mamake marehemu, ambaye alisema kuwa ni jambo la kusikitisha kwani alikuwa amezungumza na mwanaye asubuhi kabla ya tukio hilo, huku akisisitiza kuwa mwanaye hakuwa na tatizo lolote. 

Maafisa wa polisi walifika na kuchukuwa mwili hadi ufuo.