Kikundi kimoja cha wabunge kutoka mkoa wa kati sasa wametishia kumwondoa kazini Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaisery kwa kutowajibika kazini.
Watano hao na seneta mmoja wamemwelekezea kidole cha lawama waziri huyo kwa kuegemea pande moja katika maswala ya ardhi hususan yanayoguzia jamii ya Wamaasai.
Walizungumza Jumatano, baada ya wakulima wawili kuvamiwa na vijana wa jamii ya wamasai na kukatwa vibaya mwilini katika ardhi tata ya Utheri wa Lari huko Mai Mahiu.
Wabunge hao aidha wamezuru hospitali kuu ya wilaya ya Naivasha ambako wawili hao wanaendelea na matibabu.
Aidha wakuu hao wamesema kuwa ni kwa nini maafisaa wa usalama waliondolewa kwenye ardhi hiyo yenye ekari 22,000 ambapo wakulima hao walikuwa wakulima.
Wabunge hao ni pamoja na Ferdinand Waititu (Kabete), John Kihagi (Naivasha), Kimani Ngunjiri (Bahati), John Kiragu (Limuru) Mburu Kahangara (Lari) na seneta mteule Paul Njoroge.