Hatua ya daktari wa marekani kutangaza kuzinduliwa kwa 'Sauti ya Mama initiative' imepokelewa vizuri na kina mama wa kaunti ya Nyamira.
Akihutubia mamia ya kina mama kwenye uga wa Ekerenyo, afisa mshirikishi wa shirika hilo Kefa Osoro aliwahimiza kina mama kujiunga na makundi yatakayowasaidia kujiimarisha kiuchumi.
"Nilitumwa niwaambie kwamba hivi karibuni 'Sauti ya Kina mama initiative' itazinduliwa hivi na tayari daktari Joy yuko tayari kusaidia kina mama kuimarika kiuchumi na kisaikolojia, na hili tu litatimia iwapo mtajiunga kwenye makundi ili ituwie rahisi kuwasaidia," alisema Osiri.
Osiri aliongeza kwa kusema kuwa shirika hilo pia litashughulikia maswala yanayowaathiri kina mama, hasa kupigania haki zao na nafasi kwenye nyadhifa za uongozi.
Shirika hili halitawasaidia kina mama kuinua hali zao za kiuchumi bali pia litahakikisha kuwa haki za msingi za kina mama zinaheshimiwa na pia kuhakikisha kuwa kina mama wanapigania nyadhifa za kisiasa kama njia ya kuwahimiza kina mama kujua haki zao," alisema Osiri.
Mchakato huo unatarajiwa kuanzishwa katikati ya mwezi Septemba na utaonelea kina mama kufunzwa kuhusiana na ukuaji wao kisociolojia na kiuchumi.