Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kiongozi wa kundi la Mombasa Republican Council (MRC) Omar Mwamnuadzi ameachilwa kwa dhamana ya shilingi 200,000 na mahakama ya Kwale.

Hii ni baada ya Hakimu Mkaazi wa mahakama hiyo Paul Mutai kukataa ombi la mwendesha mashtaka Cecil Wakoli, la kutaka mshukiwa kunyimwa dhamana kutokana na kesi zinazomkabili mahakamani.

Mwamnuadzi alitiwa mbaroni wiki iliyopita nyumbani kwake huko Ng’ombeni na kufunguliwa mashtaka matatu ya kuwa mwanachama wa MRC, kuchanga na kupokea pesa kinyume cha sheria na kumiliki stakabadhi za kulitambulisha kundi hilo.

Akitoa uamuzi huo siku ya Jumatatu, Hakimu Paul Mutai alimuonya Mwamnuadzi na kumtaka kujiepusha na kundi hilo wakati akiwa bado anakabiliwa na kesi mahakamani.

Kesi yake itasikizwa tena mnamo Machi 28, 2016.